Ijumaa , 28th Apr , 2023

Iran hii leo imeikamata meli ya mafuta yenye bendera ya visiwa vya Marshall katika eneo la maji ya kimataifa kwenye Ghuba ya Oman.

Iran imeikamata meli ya mafuta yenye bendera ya visiwa vya Marshall katika eneo la maji ya kimataifa kwenye Ghuba ya Oman, hii ikiwa ni kulingana na jeshi la maji la Marekani, hii ikiwa ni hatua ya karibuni zaidi katika mfululizo wa kamatakamata ya meli za kibiashara katika eneo hilo katika kipindi cha miaka michache iliyopita.

Jeshi hilo limesema meli hiyo iliyokamatwa na walinzi wa pwani wa kikosi cha kimapinduzi cha Iran inavuruga usalama wa kikanda, baada ya kuzikamata karibu meli tano za biashara katika eneo la Mashariki ya Kati, kinyume cha sheria katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, huku ikiirai kuachia meli hiyo mara moja.

Mamlaka za Iran hazikutaka kuzungumzia hilo zilipotafutwa na shirika la habari la Reuters.