Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Fahamu kuhusu ujio wa DP World Tanzania

Jumatano , 7th Jun , 2023

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) baada ya taarifa zilizosambaa kuhusu bandari ya Dar es Salaam kutaifishwa huku imewataka Watanzania kupuuza taarifa za upotoshaji huo zinazodai kwamba serikali imepanga kuipa kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai kandarasi ya uendeshaji wa

shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa miaka 100.

Je, Serikali imekodisha Bandari ya Dar es Salaam kwa DP World kwa miaka 100?

Ukweli: Hakuna mkataba wowote wa ukodishaji wa Bandari ya Dar es Salaam ambao umesainiwa hadi sasa. Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Iko kwenye MAJADILIANO na DP World kuhusu uendelezaji wa bandari nchini.

Hakuna kipengele chochote kwenye makubaliano yoyote ya awali kati ya DP World na Tanzania kinachotaja ukodishaji wa miaka 100.

Je, Serikali imeuza bandari ya Dar es Salaam kwa mwekezaji wa nje?

Ukweli: Hakuna uwezekano wowote wa Serikali kuuza bandari yoyote nchini. Kinachopangwa kufanyika ni UKODISHAJI wa sehemu ya bandari ili kuongeza idadi ya shehena, ufanisi na mapato ya kodi

Je, Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kubinafsisha bandari?

Ukweli: Kumekuwa na UWEKEZAJI binafsi katika Bandari ya Dar es Salaam kupitia kampuni ya TICTS kwa takribani miaka 30, kuanzia zama za marais Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, John Magufuli hadi sasa.

Je, Kampuni ya DP World haina uwezo wowote ule na ni wababaishaji?

Ukweli: Kampuni ya DP World inamilikiwa na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). DP World ni moja ya kampuni kubwa na zinazoheshimika duniani, ambayo inaendesha bandari kwenye nchi karibu 50 duniani, ikiwemo mataifa 10 ya Afrika

DP World inaaminiwa kuendesha bandari kwenye mataifa makubwa kabisa duniani, ikiwemo Marekani, China, Ujerumani, Ufaransa na Canada. Kwa upande wa Afrika, wapo Nigeria, Afrika Kusini, Rwanda, Misri, Msumbiji na nchi nyingine

Kwa mwaka 2022 peke yake, DP World ilipata mapato ya Dola za Marekani Bilioni 17.1 na faida ya Dola Bilioni 5 (sawa na shilingi trilioni 12).

DP World imewekeza zaidi ya Dola za Marekani Bilioni 1.8 kwenye bara la Afrika katika miaka kumi iliyopita na inapanga kuwekeza Dola za Marekani Bilioni 3 (shilingi trilioni 7.2) kwenye bara hili katika miaka ijayo.

Je, Tanzania haiwezi kupata faida yoyote kutokana na uwekezaji binafsi kwenye bandari ya Dar es Salaam?

Ukweli:  Uwekezaji binafsi ni jambo la kawaida kwenye bandari nyingi kubwa Afrika, Marekani, Asia na sehemu nyingine duniani.

Tanzania inatarajia kupata manufaa yatuatayo kutokana na uwekezaji binafsi kwenye bandari ya Dar es Salaam:

(a) kuongeza fursa za ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kutokana na uwekezaji mkubwa na ongezeko la Shehena ya Mizigo itakayopitia Bandari ya Dar es Salaam;
 
(b) kuongezeka kwa ufanisi katika uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi na kuleta tija stahiki katika mnyororo wa thamani wa huduma za bandari nchini;

(c) kuongezeka kwa pato la Taifa kutokana na uboreshaji wa shughuli za kibandari;

(d) kuongeza tija na kuwezesha mwendelezo wa miradi mikubwa ya kimkakati ambayo imekuwa ikijengwa na Serikali kama vile Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), ujenzi wa meli za mizigo katika Maziwa Makuu, na Mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam; na

(e) kuchagiza na kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi (Multiplier Effect) 
zikiwemo Kilimo, Utalii, Viwanda, Mifugo, Uvuvi, Biashara na Usafirishaji na hivyo kuboresha ustawi wa Watanzania kwa ujumla.

HABARI ZAIDI

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma