
Makamu Mwenyekiti CUF Tanzania Bara, Maftaha Nachuma
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ocktoba 25, 2022 jijini Dar es salaam Makamu Mwenyekiti wa CUF Tanzania Bara Maftaha Nachuma amesema, kwa minada iliyofanyika CORECU bei ya juu mnunuzi alinunua kwa sh 1400 kwa Tani chache TU na Bei ya chini Kwa mzigo wote alinunua sh 1300 tu.
Aidha mnada uliyofanyika RUNALI bei ya juu mnunuzialinunua sh 2020 kwa kilo ambapo alitaka kwa bei hiyo Tan 300 pekee lakini bei ya chini alinunua sh 1415 kwa mzigo wote uliopo ghalani.
Pia amesema serikali inapaswa kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kuleta dawa za kupulizia mikorosho ambayo imeleta athari kwa wakulima na kusababisha mikorosho mingi kukauka.