Jumapili , 27th Nov , 2022

Wafanyabiashara ndogo ndogo na Waendesha daladala na Bodaboda wameaswa kuunda vikundi ambavyo vitawapa fursa mbalimbali za kujiinua kiuchumi na Kijamii.

Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na chuo Kikuu Mzumbe kuanzia Mwaka 2017 ambao umewasilishwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo amesema katika Sekta ya Usafirishaji na wafanyabiashara ndogo ndogo juu ya kujipatia huduma za hifadhi za jamii na bima ya Afya umeonesha asilimia 68 tuu ndio wamejiunga na vikundi.

Vikundi pia kwa wafanyabiashara ndogondogo na waendesha daladala amesema vitawasaidia kupata mikopo katika taasisi za kifedha kwani kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi ni nadra kupata mikopo katika taasisi hizo.

Utafiti huo umeonesha kuwa zaidi ya Asilimia 71 ya wafanyabiashara hao hawana namna ya kupata mikopo kwa kuwa hawana maeneo rasmi ya Kufanyia biashara na hawaaminiki kwa kuwa kila siku wanabadilisha maeneo ya Kufanyia biashara.