Jumapili , 10th Jan , 2021

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, imewakamata watu 34 wakiwemo wafanyabiashara,wanunuzi wa bidhaa na watoa huduma mbalimbali kwa kosa la kutozingatia matumizi sahihi ya mashine za Kielektroniki(Efds) ambao wametozwa shilingi milioni 58,500,000 kama adhabu,

Kaimu meneja wa mamlaka ya mapato(TRA)wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Lewis Charles.

na kati ya hizo shilingi milioni 22,580,000 zimelipwa na milioni 35,920,000 zinategemewa kulipwa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Mamlaka hiyo wilayani humo Lewis Charles, wakati akitoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu Mwaka wa fedha 2020/2021. Aidha amesema, katika mwaka wa fedha 2020/2021 TRA wilaya ya Mbinga imepewa lengo la kukusanya shilingi bilioni 3.604 na malengo hayo yatafikiwa iwapo wananchi,wafanya biashara na wadau wengine watatoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo.

Wanunuzi wote wa bidhaa mbalimbali hakikisheni mnadai risiti pindi mfanyapo manunuzi kwani ni haki ya msingi na kisheria kwa kila mnunuzi, na kutofanya hivyo ni kosa linaloweza kupelekea kupata adhabu kali ikiwemo kutozwa faini kati ya shilingi 30,000 hadi milioni 1.5”, amesema Lewis.

Amesema, mfanyabiashara atakayekamatwa kwa kosa la kutotumia mashine za Efds adhabu yake ni faini kuanzia milioni 3 na isiyozidi milioni 4.5 au kifungo cha miaka mitatu jela au vyote kwa pamoja kwa mujibu wa sheria za usimamizi wa kodi ya mwaka 2015.