'Amezaliwa May 31, Arusha lakini amekulia Dar es salaam toka akiwa mchanga hadi sasa. Anasomea Shahada ya science of business administration huko University of the People iliyopo Marekani. Ni Mkufunzi wa dansi akiwa anamiliki kampuni ya kusaidia vijana katika swala zima la kucheza na sanaa.

Kwa sasa Khalila anamiliki dance studio yake mwenyewe ambapo anaendesha mafunzo mbalimbali yanayohusu sanaa ya kucheza
Mbali ya hapo ameshafanya kazi na wasanii wakubwa kama vile Ali Kiba na Jokate. Pia ameshawahi kuwa choreographer wa maonyesho makubwa kama Namibia Annual Music Awards (NAMA).