Submitted by Brendansia on Jumatano , 9th Apr , 2014 Mashabiki wa Mafikizolo wakipiga picha ya pamoja kabla ya kuingia ukumbini. mashabiki wakionyesha mavazi ya aina mbalimbali ya kiafrika. Mtangazaji lotus Kyamba wa kipindi cha Nirvana akiwahoji mashabiki juu ya fasheni zao mbalimbali. Mashabiki wakiwa wamevalia rangi mbalimbali za kiafrika kusini. Kundi la warembo wakisubiri burudani ndani ya ukumbi wa mlimani city hall. Umati wa watu ukiwa umejikusanya kwa kupata burudani ya afrika kusini. wageni mbali mbali wakifanya mahojiano na mtangazaji na mtangazaji Deogratius kithama. wapenzi wa burudani ya muziki na redio wakionyesha uzalendo wao. wazalendo wa muziki wa kiafrika wakidumisha utamaduni na mavazi ya kiafrika. wapenzi wa burudani ya muziki wakionyesha tabasamu na fasheni mbalimbali. Ukumbi ukiwa tayari kwa ajili ya tamasha. Upande wa VIP ukiwa tayari kwa ajili ya kupokea wageni. Wauzaji wa beer ya castle lite wakiwa tayari kufanya biashara. Muimbaji Nhlanhla Nciza akikwea jukwaa ili kutoa burudani kamili. Pale burudani ilipoanza kukolea. Ama kweli uzee mwisho chalinze, Bibi akisakata mauno wakati wa tamasha akidhihirisha umri haumnyimi mtu kupata burudani ya kisasa. Bibi akionyesha ujuzi wake wa kwaito wakati wa tamasha. Theo Kgosinkwe mwimbaji wa kiume katika kundi la mafikizolo naye akiweka mabo sawa. Burudani ilipokolea na mavazi yakabadilika na kua kiafrika zaidi. Mashabiki wakionyesha kufurahishwa na burudani iliotolewa. Theo akionyesha umahiri wake wakusakata afro house na miondoko ya kwaito na kupagawisha mashabiki. madansa nao walipata nafasi ya kuonyesha ujuzi wao. Theo akitoa burudani kikamilifu. Wakicheza kwa pamoja na kufundisha mashabiki jinsi ya kucheza miondoko hiyo stejini. Wakiwashukuru mashabiki wao kwa upendo na matayarisho waliopata kwa kuwaimbia nyimbo mbalimbali. Nhlanhla Nciza akiwa stejini. Mafikizolo wakifanya mahojiano na watangazaji wa kipindi cha nirvana Deogratius Kithama na Lotus Kyamba. Tho akipozi kwa ajili ya picha katika chumba cha mahojiano. Nhlanhla akipozi kwa ajili ya picha. Mafikizolo wakiwa katika majadiliano na watangazaji wa Nirvana.