Jumanne , 8th Apr , 2014

Wasanii wa muziki Moze Radio pamoja na Weasel TV, baada ya kuachia video yao mpya ya ngoma inayokwenda kwa jina Breath Away ambayo imefanyika huko Afrika Kusini, sasa wanajifua kwa ajili ya uzinduzi wa albam yao inayokwenda kwa jina Street Lights.

Mose Radio, Weasel TV

Wasanii hawa wanaounda kundi la Goodlyf wamepanga kufanya uzinduzi huu mwezi ujao tarehe mbili huko jijini Kampala, na kuongeza idadi ya albam ambazo wamekwishazitoa kufikia 7 tangu walipoanza kufanya kazi kwa pamoja mwaka 2008.

Hatua hii inaongeza rekodi nyingine nzuri ya mafanikio katika kundi hili licha ya changamoto za hapa na pale ikiwepo tetesi za kutaka kutengana na kutokuwa na maelewano mazuri na meneja mahiri wa muziki, Jeff Kiwanuka.