Jumatano , 8th Mei , 2024

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, amewataka abiria wanaosafiri kwa kuitumia barabara ya Tunduma - Mbeya na wanaotoka nje ya mkoa wa Songwe kufunga mkanda ili kuepuka madhara ambayo yanayoweza kuepukika.

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

Kauli hiyo imetolewa wakati akifanya ukaguzi wa magari eneo la Chimbuya wilayani Mbozi na kueleza umuhimu wa kufunga mkanda pindi abiria awapo safarini ili kujihakikishia usalama wake.

"Mnatakiwa kufunga mkanda ili endapo inatokea ajali uwe salama lakini usipofunga mkanda utashindwa kujizuia na itakutoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine na kusababisha madhara kwa watu wengine kwa hiyo abiria nawaomba fungeni mkanda wakati wote unapokuwa safarini toka unapoingia kwenye gari funga mkanda, ukitoka kula na kuchimba dawa funga mkanda ili uwe salama wewe na mwingine,"- amesema SSP Bukombe.