Jumanne , 7th Mei , 2024

Japani imetengeneza historia mpya kwa kuwa nchi ya kwanza kuzindua teknolojia ya 6G, ikumbukwe Duniani kwa sasa teknolojia inayotumika na yenye kasi ni 5G ambayo yenyewe pia kwa uhalisia wake kuna baadhi ya maeneo haipatikani.

Teknolojia ya 6G ambayo imetambulishwa na Japan inatajwa kuwa na kasi ya utumiaji wa data mara 20 zaidi ya kasi inayopatikana kwenye 5G. Kasi ya sasa inayopatikana kwenye mtandao wa 5G ni 20 GB kwa sekunde, lakini kasi ya mtandao wa 6G ni 1TB kwa sekunde.

kwa urefu zaidi kuhusiana na teknolojia hii ya 6G usikose kusikiliza SUPATECH kila siku Jumatatu - Ijumaa 12:00 Asubuhi, kupitia EastAfricaRadio pekee.