Amezaliwa Tarehe 10/06 Mwanza na kukulia ndani ya jiji la Dar es Salaam, amesoma shule ya Esaacs Primary School na Kampala International High School. Tbway ana urefu wa futi 6.5 . Anapenda sana kupiga picha, kuogelea, movie na kuendesha magari kwa kasi. Alipachikwa jina la TBWAY 360 akiwa na umri wa miaka 14 baada ya kuzungusha gari mzunguko wa duara yaani nyuzi 360. Pia ni mtangazaji wa kipindi maarufu Tanzania cha vijana especially walio shuleni cha EATV 5Selekt.