Jordan Clarkson aachana na Utah Jazz
Mkongwe wa timu ya Utah Jazz inayoshiriki ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA, Jordan Clarkson, ameachana rasmi na klabu hiyo, ambapo hivi sasa ni mchezaji huru na yuko kwenye makubaliano ya kujiunga na New York Knicks.