Mwakyembe akana nukuu potofu za vitabu vyake
Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Dakta Harrison Mwakyembe ameelezea kusikitishwa kwake na nukuu zilizofanywa na baadhi ya wajumbe walipojaribu kunukuu vitabu alivyoandika yeye na Prof Issa Shivji kuwa walikuwa wakipendekeza muundo wa serikali tatu.