Wednesday , 23rd Apr , 2014

Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Dakta Harrison Mwakyembe ameelezea kusikitishwa kwake na nukuu zilizofanywa na baadhi ya wajumbe walipojaribu kunukuu vitabu alivyoandika yeye na Prof Issa Shivji kuwa walikuwa wakipendekeza muundo wa serikali tatu.

Mjumbe wa bunge maalumu la katiba Dkt Harrison Mwakyembe

Katika kikao cha Bunge cha majadiliano ya mapendekezo ya kamati kuhusu Sura Mbili za Rasimu ya katiba, Mwakyembe amesema kuwa, vijana wanaonukuu vitabu vyake hawanabudi kusoma kwa kina nakuelewa badala ya kukurupuka na kusoma mstari mmoja na kisha kuutumia.

Mwakyembe ameungana na wajumbe wenazake kutoka chama cha mapinduzi CCM kutaka muungano wa serikali mbili kwa madai kuwa serikali tatu zitasababisha mzigo wa gharama za uendeshaji kwa wananchi.