Bunge latakiwa kuchunguza mikataba tata ya madini
Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imeitaka serikali kuunda kamati teule ya bunge kuchunguza mikataba inayotiliwa shaka na wabunge kuwa kuna ufisadi umefanyika ukiwahusisha viongozi mbalimbali wa serikali katika Wizara ya Nishati na Madini.

