Friday , 30th May , 2014

Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imeitaka serikali kuunda kamati teule ya bunge kuchunguza mikataba inayotiliwa shaka na wabunge kuwa kuna ufisadi umefanyika ukiwahusisha viongozi mbalimbali wa serikali katika Wizara ya Nishati na Madini.

Waziri kivuli wa nishati na madini nchini Tanzania, mbunge wa Chadema John Mnyika.

Akitoa hotuba ya maoni ya Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Waziri kivuli wa wizara hiyo, Mhe. John Mnyika amesema upotevu mkubwa wa fedha za serikali unachangiwa na mikataba isiyoridhisha.

Nao wabunge mbalimbali wakichangia hotuba hiyo wamesema fedha nyingi zimetoroshwa kutokana na viongozi kutosimamia uwazi na uwajibikaji pamoja na kutowajali wachimbaji wadogo wa madini kwa manufaa ya wananchi wote.