Young Killer aangalia viwango tu
Staa wa muziki Young Killer, aliyejijengea kutokutabirika katika aina ya wasanii ambao huwa anawashirikisha katika ngoma zake, ameweka wazi kuwa, huwa anazingatia zaidi uwezo wa mtu na kile ambacho kitawezesha ngoma yake kudumu kwa muda mrefu.