Monday , 24th Aug , 2015

Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtwara mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hasnain Murji, amesema atawafikisha mahakami wananchi watakaothubutu kuwazomea wanachama wa CCM wanaovaa sare za chama na kutembea mitaani.

Mbunge wa Mtwara Mjini Ndugu Hasnain Murji akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM ulivyotekelezwa vizuri kwenye mkutano wa hadhara

Hatua hiyo imekuja baada ya malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wanachama wa chama hicho katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni kwa mgombea huyo, uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mtakatifu Augustine (SAUT) tawi la Mtwara.

Hali imekuja baada ya wanachama wa chama hicho kuzomewa baadhi maeneo ya mijini pindi wanapoonekana wakiwa wamevalia mavazi hayo ya njano na kijani kirahisi ambacho kinawafanya kuingia uwoga kuonesha mapenzi yao kwa chama hicho.

Aidha, amewataka wanachama kutomuangusha katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na ahadi ambayo aliitoa mbele ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea mkoani humo kuzindua miradi mbalimbali, kwamba Mtwara ndiyo mkoa ambao utampa kura nyingi mgombea wa urais wa chama hicho Dkt. John Magufuli.