Shinzo Abe amuahidi ushirikiano Dkt. Magufuli
Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Shinzo Abe amemtumia salamu za pongezi Rais wa Tanzania kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa awamu ya tano na kumuahidi kuwa Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na maendeleo.