JKU yapita bila jasho Kombe la Shirikisho Afrika
Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) imefanikiwa kuingia hatua ya pili ya mashindano ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupata ushindi wa mezani kufuatia wapinzani wao Timu ya Gaborone United kutoka Botswana kujiondoa katika mashindano.

