Wachezaji wa Simba Ibrahim Ajibu na Jamal Mnyate wakishangilia bao la kwanza.
Klabu ya soka ya Simba imezidi kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji ya Songea jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.