UNHCR yahofia hatma ya msemaji wa Riek Machar
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR lina wasiwasi mkubwa kuhusu hatma ya msemaji wa Riek Machar nchini Kenya, James Gatdet Dak ambaye alipewa amri ya kuondoka nchini humo tarehe pili mwezi huu kurejea Juba, Sudan Kusini.