Vifo vya uzazi bado tishio nchini Tanzania
Imeelezwa kuwa kati ya wanawake 100,000 wanajifungua kwa mwaka nchini Tanzania, wanawake 432 hupoteza maisha kutokana na changamoto mbalimbali katika sekta ya afya hasa ukosefu wa huduma bora na zile za dharura pamoja na upungufu wa wauguzi wakunga.