Simba kuikamua Yanga milioni 50 za Hassan Kessy
Shirikisho la Soka Tanzania TFF limeiamuru klabu ya Yanga kuilipa Simba shilingi milioni 50 kama fidia ya kukiuka utaratibu wa usajili wa mchezaji Hassan Ramadhani Kessy pamoja na kuitoza faini ya shilingi milioni 3.
