Wafaransa watoa bilioni 25.7 kusaidia nishati TZ
Juhudi za serikali za kujenga uchumi wa viwanda zinaendelea kuungwa mkono na wadau wa ndani na nje ya nchi baada ya Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD hii leo kusaini makubaliano yaliyowezesha upatikanaji wa shilingi za Tanzania bilioni 25.67.