Askari 300 waandaliwa Simba na Yanga
Kuelekea mchezo ujao wa watani wa jadi katika soka la Bongo, Simba na Yanga utakaopigwa Jumamosi ya tarehe 25/02/2017 katika dimba la Taifa Dar es Salaam, serikali imeonya mashabiki watakaofanya vurugu, huku askari 300 wakiwa wameandaliwa.