CCM yamtolea nje Wema Sepetu
Baada ya Muigizaji Wema Sepetu kutangaza kurudi ndani ya Chama Cha Mapinduzi baada ya kukihama Februari mwaka huu, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa chama hicho hakina taarifa yoyote ya kurudi kwa Wema Sepetu.