Serengeti Boys kushiriki michuano ya UEFA
Shirikisho la Soka Tanzania TFF limetangaza kuwa Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania U17 “Serengeti Boys” itashiriki kwenye mashindano maalumu ya maandalizi ya Afcon U17 yatakayofanyika Antalya nchini Uturuki mapema mwakani.