Boti ya uwokozi yaanza majaribio
Boti mpya ya kisasa ya uokozi na matibabu (Modern Ambulance Boat) imezinduliwa kwa kushushwa majini na kufanyiwa majaribio kati ya jiji la Mwanza na kisiwa cha Ukerewe. Hatua hii ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza rasmi kutoa huduma kwa wananchi wanaozunguka Ziwa Victoria.