Wanafunzi Vyuo vya Ufundi wengi walifeli Form 4
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya REPOA umebaini kuwa wanafunzi wengi wanaosoma katika Vyuo vya Ufundi Stadi, hawana elimu ya kutosha na wengi wao ni wale, waliofanya vibaya kuanzia Shule ya Msingi na hata Kidato cha 4, hali inayopelekea elimu yao kutokidhi mahitaji ya soko la ajira.