Mwanafunzi aliyetoa laki 9 kwa ajili ya GPA adakwa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mkoani Dodoma, inamshikilia mwanafunzi wa mwaka wa tatu, katika chuo kikuu cha St John's mkoani humo, James Kwangulija kwa kosa la kujaribu kutoa hongo ya laki tisa kwa afisa mitihani ili asaidie kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wenzake 6.