Askari JWTZ afungwa miaka 3 kisa wivu wa mapenzi
Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) kikosi cha KJ 843, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, Shabani Mkondya (34) amehukumiwa kifungo cha miaka 3 Gerezani, baada ya kukutwa na hatia ya kumjeruhi mkazi wa Kata ya Nyangao, Ramadhani Mussa, kutokana na wivu wa kimapenzi.