Ndugai azungumzia hali ya Mbunge aliyepata Corona
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema kuwa hali ya Mbunge wa kwanza aliyetangazwa kuwa amepata maambukizi ya Virusi vya Corona, inaendelea vizuri na kwamba hana dalili zozote za maambukizi hivyo anangoja vipimo vya mwisho ili aweze kuruhusiwa.