Mbunge aomba kifunguliwe chuo cha wizi
Mbunge wa Kahama Mjini kupitia CCM Jumanne Kishimba, ameiomba Serikali ifungue chuo cha wizi kwa kuwa matukio ya wizi katika sekta za umma na Halmashauri nyingi umeshamiri kwa kiasi kikubwa na kwamba chuo hicho kitasaidia wale watu wanaoenda kuchunguza wezi, kuzijua mbinu zao na kuwabaini.