CHADEMA waeleza hali ya Mbowe kwa sasa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe anaendelea kupata uangalizi wa ziada chini ya Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Aga Khan, baada ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya ziada tangu alipofikishwa hospitalini hapo.