Vijana wa ACT Wazalendo kumuandikia Membe barua
Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT Wazalendo imesema kuwa itamuandikia barua aliyewahi kuwa waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, ili aweze kujiunga na chama hicho kwa kile wanachoamini kuwa na yeye ni muhanga wa demokrasia.

