Katambi afika kwenye msiba wa aliyefia ndani
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu, Patrobas Katambi, ambaye ni mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini, amefika kwenye msiba wa Wande Kulwa mwenye ualbino mkazi wa Nhelegani, aliyekutwa amefariki nyumbani kwake takribani siku tano.