Wednesday , 19th Nov , 2025

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa onyo kali kwa viongozi wa serikali na watendaji wa umma, kikisema kitawachukulia hatua kali wale wote watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

''Chama kimejipanga kikamilifu kuhakikisha maono na matarajio ya Rais Samia Suluhu Hassan yanatekelezwa kikamilifu katika ngazi zote za utawala''

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma Jumatano, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi, amesisitiza kuwa serikali inatarajiwa kufanya kazi kwa kasi mpya na kwa kuzingatia viwango vya juu vya uwajibikaji ili kufikia malengo ya kitaifa.