Ukijiandikisha mara mbili utapelekwa mahakamani
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imewatahadharisha wananchi wenye nia ya kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye daftari la kudumu la wapiga kura watapigwa faini kuanzia shilingi 100,000/= na isiyozidi shilingi 300,000/=, au kifungo kuanzia miezi 6 na isiyozidi miaka miwili au vyote pamoja.