Zanzibar kujenga kiwanja kipya AFCON2027

Mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka wa 2027 yanatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa ushirikiano nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda ambazo ndizo zitakuwa  nchi wenyejiwa mashindano hayo.

Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali yake ina mpango wa kujenga kiwanja cha mpira wa miguu cha kimataifa kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 zitakazofanyika nchi tatu za Afrika Mashariki.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS