Ansu Fati kukaa nje ya uwanja wiki nne

Nyota huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 22 amekuwa muhanga wa majeraha ya mara kwa mara hivyo kufifisha kiwango chake cha uchezaji alichokionyesha akiwa na umri wa miaka 16 wakati anapandishwa kucheza kikosi cha kwanza cha Barcelona. Fati alitabiriwa makubwa ndani ya Catalunya mpaka kupewa jezi namba 10 iliyovaliwa na nyota kama Ronaldinho Gaucho na Lionel Messi ambaye alihamia  PSG ya Ufaransa. 

Mchezaji wa klabu ya Barcelona ya Hispania Ansu Fati atakaa nje y uwanja kwa kipindi kisichopungua wiki nne baada ya kuumia misuli akiwa mazoezini.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS