Nyota huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 22 amekuwa muhanga wa majeraha ya mara kwa mara hivyo kufifisha kiwango chake cha uchezaji alichokionyesha akiwa na umri wa miaka 16 wakati anapandishwa kucheza kikosi cha kwanza cha Barcelona. Fati alitabiriwa makubwa ndani ya Catalunya mpaka kupewa jezi namba 10 iliyovaliwa na nyota kama Ronaldinho Gaucho na Lionel Messi ambaye alihamia PSG ya Ufaransa.
Mchezaji wa klabu ya Barcelona ya Hispania Ansu Fati atakaa nje y uwanja kwa kipindi kisichopungua wiki nne baada ya kuumia misuli akiwa mazoezini.
Nyota huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 22 amekuwa muhanga wa majeraha ya mara kwa mara hivyo kufifisha kiwango chake cha uchezaji alichokionyesha akiwa na umri wa miaka 16 wakati anapandishwa kucheza kikosi cha kwanza cha Barcelona. Fati alitabiriwa makubwa ndani ya Catalunya mpaka kupewa jezi namba 10 iliyovaliwa na nyota kama Ronaldinho Gaucho na Lionel Messi ambaye alihamia PSG ya Ufaransa.
Majeruhi haya yamempata kipindi ambacho Kocha Hansi Flick akijaribu kumpa nafasi kwenye timu yake baada ya msimu uliopita kukitumikia kikosi cha Brighton & Hove Albion F.C. kinachorishiki ligi kuu ya Uingereza kwa mkopo wa msimu mzima.Anatajwa kuwa mmoja wa Wachezaji wenye kiwango bora sana kutokea Akademi ya La Masia iliyozalisha Xavi Hernandes, Andres Iniesta , Carles Puyol,Victor Valdes,Sergio Busquets,Pep Guardiola,Lionel Messi,Gavi na Lamine Yamal.
Ansu Fati akiwa fiti kucheza bila wasiwasi wa majeruhi ni Winga hatari kutokana na uwezo wake wa kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha anakasi na uwezo mkubwa wa kufunga kutokea upande wowote uwanjani,kuumia kwake kunamfanya kupoteza kujiamini hivyo kupoteza baadhi ya sifa zinazomfanya kuwa na hatari uwanjani.
Kuna baadhi ya Wachezaji walibarikiwa vipaji vikubwa vya kucheza soka lakini walishindwa kufukia matarajio ya Wadau wengi wa mpira wa miguu Duniani baada ya kukatisha safari yao ya kucheza mpira kulikosababishwa na majeruhi. Abou Diaby,Jack Wilshere,Andre Schurrle, majina machache ya Wachezaji waliolazimika kumaliza safari zao za kucheza mpira kutokana na majeraha ya mara kwa mara ninachelea kusema kama Ansu Fati akiendelea na muendelezo wa kuumia sitoshangaa akitangaza kustaafu kucheza mpira wa miguu.
Ijapokuwa kuna Wachezaji ambao waliandamwa namajeraha wakiwa na umri mdogo ila wakaja kutengemaa walipofika umri wa utu uzima na kucheza kwa mafanikio na kushinda mataji na vilabu walivyovitumikia.Gareth Bale,Marco Reus,Arjen Robben na Robin van Persie majina ya Wachezaji ambao walikumbwa na majereha lakini vilabu vyao viliwavumilia na kucheza kwa viwango vikubwa sambamba na kushinda mataji makubwa Ansu Fati anaweza kutengemaa mbeleni na kuishi ndoto zake kuwa nguli wa ndani ya Barcelona.