Akutwa amejinyonga mkoani Kilimanjaro
Mwanaume anayefahamika kwa jina la Hassan Ali anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 mkazi wa Pasua mkoani Kilimanjaro, amekutwa amefariki dunia kwa kile kinachohisiwa kuwa ni kujinyonga kwa kamba za katani pembezoni mwa uwanja wa Nelson Mandela, Pasua mjini Moshi.