Friday , 5th Jun , 2015

Young Dee amesema kuwa rekodi yake mpya ya Cowbama, imetoka sasa kama kazi yake rasmi kuonesha heshima na shukrani kwa mchango wa marehemu katika muziki wake.

Young Dee

Young Dee amesema kuwa rekodi yake mpya ya Cowbama, ambayo ni maalum kwa ajili ya kumuenzi marehemu Albert Mangwair ni kazi ambayo alikuwa nayo toka miaka 2 iliyopita, na imetoka sasa kama kazi yake rasmi kuonesha heshima na shukrani kwa mchango wa marehemu katika muziki wake.

Young Dee ameiambia eNewz kuwa, hakutaka kutoa rekodi hii katika kipindi kile cha msiba kutokana na kutotaka iwe moja ya kazi za mpito ambazo hufanywa kuwaenzi marehemu, lengo lake kuiachia sasa ikiwa ni kutaka iishi zaidi kama kazi zake nyingine rasmi.

Young Dee amesema pia kazi hii kiuhalisia ilikuwa iwe ni kolabo kati yake na Marehemu Mangwair, na walikuwa wamepanga kuifanya baada ya yeye kurejea kutoka safari yake na Afrika Kusini, mpango ambao ulizima baada ya mauti kumfika staa huyo aliyekuwa mkali wa miondoko huru.