Friday , 15th May , 2015

Uongozi wa Chama cha Mpira wa Wavu mkoa wa Dar es salaam DAREVA, umepenga kutumia michezo ya shule za sekondari UMISSETA kusaka wachezaji watakaounda timu itakayoshiriki mashindano ya kanda.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa DAREVA, Yusuph Mkarambati amesema wanatarajia kutumia mashindano ya sekondari wilaya ya Kinondoni kusaka wachezaji watakaounda timu mbalimbali za michezo.

Mkarambati amesema, mashindano hayo yaliyoanza kutimua vumbi hapo jana kwa kushirikisha shule za Kinondoni yanalenga kupata timu ya wilaya itakayopambana na timu kutoka wilaya ya Ilala na kupata wachezaji watakaounda timu ya Kanda ya Dar es salaam.

Mkarambati amesema, michezo hiyo itawapa fursa walimu wa michezo na wajumbe wa kamati za ufundi za vyama vya michezo kushirikiana na kuwachagua wachezaji wenye viwango ambao wataleta ushindani.