Friday , 1st May , 2015

Staa wa muziki Jaguar kutoka nchini Kenya ameingia kwa mara nyingine katika vichwa vya habari baada ya kuchangia kiasi cha shilingi laki 2 za Kenya, zaidi ya shilingi milioni 4 za kitanzania katika harusi ya rafiki yake.

Msanii wa muziki wa nchini Kenya Jaguar

Mchango wa Jaguar kwa mdau wake mkubwa wa burudani kutoka Mombasa, Hassan Faisal aka ‘Mr President unaingia kama nakshi kujazia bajeti ya shilingi milioni 3 za Kenya katika harusi hiyo, pesa ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 62 za kitanzania.

Mchango huo unakuwa ni alama nyingine ya moyo mzuri wa msanii huyo kupenda kushirikiana na watu katika shida na raha, akiwa pia na rekodi ya kushiriki katika kusaidia wale walio katika mazingira magumu kutoka sehemu mbalimbali huko nchini Kenya.