Monday , 20th Apr , 2015

Msanii wa muziki Jaguar kutoka nchini Kenya, baada ya kumaliza onesho lake huko Georgia Marekani amerushiwa lawama na mashabiki kutokana na kuchelewa katika onesho na kutumia muda mfupi kutumbuiza kabla ya kuondoka jukwaani.

msanii wa muziki nchini Kenya Jaguar akiwa Georgia Marekani

Kupitia baadhi ya maoni ya mashabiki waliohudhuria onesho hilo, Jaguar alitakiwa kuanza kutumbuiza saa nne na badala yake akafika ukumbini saa 8 na nusu usiku na kutumbuiza kwa dakika 26 tu, hatua ambayo ni sawa na kuwaibia pesa walizolipa kama viingilio.

Kwa njia ya mtandao Jaguar amejibu tuhuma hizo kwa kurusha lawama kwa moja ya wanahabari wa Kenya anayefanya kazi nchini Marekani kwa kusambaza taarifa hizo baada ya yeye kukataa kufanya naye mahojiano.