Kauli hii ya Baby J inakuja akiunga mkono kampeni ya ZamuYako2015 kuhamasisha kundi hilo muhimu ndani ya jamii kushiriki katika uchaguzi, akiamini kuwa kushiriki kwa wingi na usawa katika kupiga kura ni kitu ambacho kinachangia pia kudumisha amani katika nchi.
Tuesday , 14th Apr , 2015
Staa wa muziki Baby J kutoka Zanzibar, ameongea na vijana kutoka Tanzania Visiwani na Tanzania Bara kwa ujumla kuwa mstari wa mbele na kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kushiriki katika zoezi la upigaji kura mwaka huu.