Tuesday , 14th Apr , 2015

Serikali imeagiza Wakurugenzi wa halamshauri manispaa na majiji kuwachukulia hatua walimu wakuu waliotangaza kufungwa kwa shule kutokana na ukosefu wa chakula kwa kuwa hawakufuata taratibu.

Katibu mkuu wa Wizara ya Tamisemi Jumanne Sagini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaama Katibu mkuu wa wizara ya TAMISEMI Jumanne Sagini amesema kuwa walimua hao hawakustahili kutangaza kufungwa shule wangewasiliana na wakurugenzi ambao ndio wenye mamlaka huku akisisitiza kuwa pesa tayari zilisha pelekwa katika akaunti za Halmashauri.

Akizungumzia kuhusu malipo ya wazabuni ambao wanadaiwa kugomea kusambaza chakula kutokana na kutolipwa pesa zao amesema kuwa tangu Julai Mwaka jana hadi Machi mwaka huu serikali imelipa zaidi sh bilioni 28.1 sawa na asilimia 66.7 ya madeni ya wazabuni.

Sagini amesema ameshangazwa na kusikia kuwa shule zimefungwa kutokana na kukosa chakula wakati fedha zimeshapelekwa kwenye halmashauri zao na kushangazwa na kusikia kuwa wazabuni hao hawajalipwa.