Monday , 13th Apr , 2015

Mchekeshaji mahiri kutoka nchini Uganda, Anne Kansiime anatarajiwa kwenda kuwavunja mbavu watu huko Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi ujao, katika sherehe kubwa za tuzo za Star Qt za mwaka huu.

mchekeshaji maarufu wa nchini Uganda Anne Kansiime

Tukio hilo kubwa litafanyika ndani ya Jiji la Johannesburg, na hii ikiwa ni moja ya maonyesho makubwa ya Kansiime ndani ya Afrika.

Tuzo za StarQt kwa mwaka huu zinatarajia kuwatuza wafanyabiashara, wanamitindo, wasanii, taasisi za kielimu na watu binafsi ambao wameonyesha utofauti na mafanikio ya kipekee katika kazi zao kutoka huko Afrika Kusini.